Home SPORTS Taifa Stars yaipigia hesabu Madagascar

Taifa Stars yaipigia hesabu Madagascar

0

KIM Poulsen, Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania,Taifa Stars amesema kuwa kwa sasa akili zote ni kuelekea mchezo wao ujao wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Madagascar.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Septemba 7, Uwanja wa Mkapa majira ya saa 10:00 jioni.

Michuano ya Kombe la Dunia inatarajiwa kufanyika nchini Qatar 2022. Stars itashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya DR Congo kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa TP Mazembe.

Kim amesema:”Tumerejea Tanzania na tunaenda kujiandaa na mchezo unaofuata ambao ni dhidi ya Madagascar tukiwa uwanja wa nyumbani tutapambana ili kuweza kupata nafasi ya kufuzu.

“Kwa mchezo wetu uliopita ninawapongeza wachezaji kwa kuwa walipambana bila kukata tamaa hivyo nina amini kwa mchezo ujao pia watafanya vizuri,”.

Tayari Stars imeanza maandalizi kwa ajili ya mchezo wao huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Previous articleVIDEO :Annastacia M.Kakii – Pack and Go
Next articleSoldiers Say Guinea Constitution, Gov’t Dissolved in Apparent Coup

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here